Isaiah 33

Taabu Na Msaada


1 aOle wako wewe, ee mharabu,
wewe ambaye hukuharibiwa!
Ole wako, ee msaliti,
wewe ambaye hukusalitiwa!
Utakapokwisha kuharibu,
utaharibiwa;
utakapokwisha kusaliti,
utasalitiwa.


2 bEe Bwana, uturehemu,
tunakutamani.
Uwe nguvu yetu kila asubuhi
na wokovu wetu wakati wa taabu.

3 cKwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia;
unapoinuka, mataifa hutawanyika.

4 dMateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,
kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.


5 e Bwana ametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,
ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

6 fAtakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,
ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;
kumcha Bwana ni ufunguo wa hazina hii.


7 gAngalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani,
wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

8 hNjia kuu zimeachwa,
hakuna wasafiri barabarani.
Mkataba umevunjika,
mashahidi wake wamedharauliwa,
Au: miji yake imedharauliwa.

hakuna yeyote anayeheshimiwa.

9 jArdhi inaomboleza
Au: Ardhi inakauka.
na kuchakaa,
Lebanoni imeaibika na kunyauka,
Sharoni ni kama Araba,
nayo Bashani na Karmeli
wanapukutisha majani yao.


10 l“Sasa nitainuka,” asema Bwana.
“Sasa nitatukuzwa;
sasa nitainuliwa juu.

11 mMlichukua mimba ya makapi,
mkazaa mabua,
pumzi yenu ni moto uwateketezao.

12 nMataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,
kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”


13 oNinyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;
ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu!

14 pWenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,
kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:
“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?
Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

15 qYeye aendaye kwa uadilifu
na kusema lililo haki,
yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma
na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,
yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,
na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

16 rhuyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,
ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.
Atapewa mkate wake,
na maji yake hayatakoma.


17 sMacho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake
na kuiona nchi inayoenea mbali.

18 tKatika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:
“Yuko wapi yule afisa mkuu?
Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?
Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”

19 uHutawaona tena wale watu wenye kiburi,
wale watu wenye usemi wa mafumbo,
wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.


20 vMtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;
macho yenu yatauona Yerusalemu,
mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa,
nguzo zake hazitang’olewa kamwe,
wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.

21 wHuko Bwana atakuwa Mwenye Nguvu wetu.
Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.
Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,
wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

22 xKwa kuwa Bwana ni mwamuzi wetu,
Bwana ndiye mtoa sheria wetu,
Bwana ni mfalme wetu,
yeye ndiye atakayetuokoa.


23 yKamba zenu za merikebu zimelegea:
Mlingoti haukusimama imara,
nalo tanga halikukunjuliwa.
Wingi wa mateka yatagawanywa,
hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.

24 zHakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;
nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.
Copyright information for SwhKC